TIMU
ya Azam FC na Mbeya City zimeendelea kuifukuzia Yanga kileleni mwa
msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya zote kuibuka na ushindi wa
bao 1-0.
Azam
iliifunga Mtibwa Sugar uwanja wa Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es
Salaam, huku Mbeya City ikiichapa Kagare Sugar mjini Bukoba.
Ushindi
huo umezifanya Azam na Mbeya City zote kufikisha pointi 30, moja nyuma
ya Yanga yenye pointi 31 baada ya kushuka dimbani mara 14.
Katika
mchezo wa Azam na Mtibwa, timu zote zilianza kwa kushambuliana kwa
zamu, huku Azam ikionekana kulisakama lango la Mtibwa kwa kasi zaidi,
lakini uimara wa mabeki wake waliweza kukoa hatari kadhaa.
Pasi
iliyopigwa na Joseph Kimwaga iliweza kumpata vizuri, Tchetche
aliyefunga bao hilo pekee baada ya kuweza kuwachomoka mabeki wa Mtibwa
na kufumua shuti lililojaa moja kwa moja wavuni.
Kikosi
cha Azam kilikuwa; Mwadini Ali, Malika Ndeule, Erasto Nyoni, Said
Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure
Boy’, Brian Umony/Ismael Kone dk13/Khamis Mcha dk71, Kipre Tchetche na
Joseph Kimwaga/Seif Karihe dk69.
Mtibwa
Sugar; Hussein Sharrif, Hassan Ramadhani, Said Mkopi, Salim Mbonde,
Salvatory Ntebe, Shaaban Nditi, Shaaban Kisiga, Masoud Ally/Abdallah
Juma dk62, Juma Luizio/Mussa Mgosi dk84, Jamal Mnyate na Vincent
Barnabas/Mohamed Salum dk75.
Katika
mchezo mwingine, Coastal Union ilitoka sare ya kufungana bao 1-1, JKT
Oljoro mchezo uliopigwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga
0 comments:
Post a Comment