Karagwe. Baadhi ya abiria Mji Mdogo wa Kayanga
na wamiliki wa daladala, wamelalamikia uongozi wa Halmashauri ya Karagwe
kushindwa kutengeneza miundombinu ya stendi ya wilaya miaka 50
iliyopita tangu wilaya kuanzishwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya abiria
walionyesha kukerwa na magari kujipanga kandokando barabara kutokana na
ubovu wa stendi.
Selian Katabazi alisema utaratibu unaotumiwa wa kuegesha magari kandokando ya barabara, ni hatari kwa maisha ya watu.
Katabazi alisema inashangaza kuona makao makuu ya
wilaya ambayo imeanza miaka 50 iliyopita, ikiwa imeongozwa na wakuu wa
wilaya 21 na wakurugenzi 14 haina miundombinu ya kuridhisha.
Nao wamiliki wa daladala, walisikitishwa na
halmashauri kuendelea kukusanya ushuru katika stendi ambayo haikidhi
vigezo. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Bosco Ndunguru
akijibu swali la Diwani wa Kata ya Kayanga, Adventina Kahatano (CUF)
alipotaka kujua hatua ya makao makuu ya wilaya kutokuwa na stendi,
alisema itapangiwa bajeti mwaka ujao wa fedha na kukukiri kuwa
haikuwekwa kwenye vipaumbele vya bajeti mwaka huu.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment