Mfuko
wa Pensheni wa PSPF unapenda kuutaarifu Umma kuwa umezindua Mpango Mpya wa
uuzaji nyumba zake zilizojengwa kwa ajili ya makazi katika mikoa ya Dar es
Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang’amba), Shinyanga
(Ibadakuli) na Iringa (Mawelewele).
Bei
za nyumba ni kati ya sh. 52,000,000.00 hadi sh. 71,000,000.00 (bila VAT). Bei
hizi ni kulingana na ukubwa wa nyumba na mkoa nyumba ilipo. Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili
hadi vinne.
Chini
ya utaratibu huu mpya unaoanza kutumika kuanzia Februari 2014; Muombaji
atapaswa kuainisha kwenye fomu ya maombi aina ya nyumba anayohitaji na Mkoa
ilipo. Malipo yanaweza kufanyika kwa
njia zifuatazo:
1)
UNUNUZI
KAMA MPANGAJI (HIRE PURCHASE):
Mnunuzi
atalipia kwa mpango wa mwezi mmoja mmoja au miezi mitatu kwa mkupuo (installments)
kulingana na thamani ya nyumba. Katika mpango huu, mnunuzi anaweza kulipia
kutokana na vyanzo vingine vya mapato yake mbali na mshahara wake. Mwanachama
wa PSPF aliyechangia chini ya miaka
mitano (5) atatakiwa kulipia kiasi cha sh.
5,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba na asiye mwanachama wa PSPF
atatakiwa kulipia kiasi cha sh.
10,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba kukidhi vigezo vya kununua
nyumba (kama mpangaji).
Mpango
huu wa Ununuzi kama Mpangaji (Hire Purchase) utamwezesha mnunuzi kulipa kati ya
sh. 450, 000.00 (laki nne na hamsini
tu) na
sh. 813,000.00
(laki nane na kumi na tatu tu) kwa mwezi kama malipo ya nyumba zinazouzwa na Mfuko
kulingana na ukubwa na eneo nyumba ilipo.
2)
MALIPO
YA MARA MOJA (OUTRIGHT PURCHASE)
Mnunuzi
atalipia gharama ya kununua nyumba kupitia akaunti ya Mfuko na kisha kusaini
makubaliano kabla ya kuhamishiwa umiliki (transfer).
3)
MKOPO
WA NYUMBA KUPITIA BENKI (MORTGAGE BASIS):
Mnunuzi
anaweza kuchukua mkopo katika mojawapo ya Benki ambazo Mfuko wa PSPF ina
mikataba nazo na kutumia mkopo huo kununulia nyumba. Mabenki hayo ni; CRDB,
Azania, Exim na NMB.
MUHIMU! Iwapo
utanunua nyumba kupitia mkopo wa benki (Mortgage) utapaswa kuwa umesajiliwa kwenye
Mfuko na kuchangia kwa muda wa miaka mitano au zaidi. Muda wa kurejesha mkopo
ni mpaka miaka ishirini na mitano (25) kulingana na matakwa ya Benki husika.
Mwombaji anayehitaji kuona au kukagua
nyumba awasiliane nasi kupitia simu: +255 22 2120912/52 au +25522 2127375-6 au
E-mail: pspf@pspf-tz.org.
Kwa maelezo zaidi fika Makao Makuu ya PSPF
yaliyopo jengo la Golden Jubilee Towers, Barabara ya Ohio au ofisi zetu
zilizopo katika kila mkoa.
Imetolewa na
Mkurugenzi
Mkuu,
Mfuko
wa Pensheni wa PSPF
0 comments:
Post a Comment