Kyerwa. Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu
Fabian Massawe ametangaza kuanzisha jitihada za kudhibiti ugonjwa wa
mnyauko unaoathiri migomba unaoenea kwa kasi Wilaya ya Kyerwa, Mkoa wa
Kagera,
Hatua hiyo ilitangazwa na Ofisa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa juzi, Stella Ndea na kwamba inatarajia kuanza wiki ijayo.
Alikuwa akizungumza na wakulima wa vijiji vya Rutunguru na Kihanga, wilayani Kyerwa.
Ndea alisema tayari sheria ndogondogo zimetungwa
kudhibiti watu watakaoshindwa kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu wa
kilimo, ambao ni kukata migomba ambayo iimeathirika.
Ndea alisema licha ya sheria hizo, ofisi ya mkuu
wa mkoa imejiandaa kuendesha Operesheni Tokomeza Mnyauko itakayohusisha
wilaya zote za mkoa na itahitimishwa Juni mwaka huu.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment